Utafahamu kuwa miezi miwili nyuma kuna wimbo ulivuja kutoka kwenye
maktaba ya Ommy Dimpoz na baada ya saa chache alitoa ombi kwa vyombo vya
habari kutocheza wimbo huu kwani haukuwa kwenye mpango wa kutoka muda
ule.
Kwenye Exclusive Interview na chombo flani cha habari,
Msanii Ommy Dimpoz amesema ni miezi nane sasa hajatoa wimbo toka Tupogo
itoke na ni muda mrefu kukaa kimya, kabla ya mwisho wa mwezi wa Nne
anampango wa kutoa wimbo mpya utaoitwa “Ndagushima”.
“Ndagushima” ni neno la lugha ya Kiha inayotumiwa zaidi Kigoma na
Linex ndiye amemsaidia kupata wazo hilo. “Ndagushima” maana yake ni
“Nakupenda Sana” au ” I'm in love With You”. Ni Neno linalotumika kama
unataka kuonyesha mapenzi mazito na ya ukweli zaidi.
Dimpoz amethibitisha Kuwa wimbo unatoka ndani ya mwezi wa nne na video alifanya Uingereza nayo inatoka.
Kuhusu kuchelewa kwa video ya Tupogo, Dimpoz amesema anapishana muda
wa kazi na J Martins ndio maana mpaka leo hawaja shoot video ya hit song
Tupogo.
Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment