Jina la Diamond Platinumz mtoto wa Tandale mwenye historia ya kuishi
maisha ya ukata, sasa hivi ni moja kati ya majina makubwa kimuziki
barani Afrika huku akishiriki kwenye project kubwa kama One Campaign
iliyoongozwa na D’Banj huku akipewa mashavu na wasanii wakubwa wa Afrika
Magharibi.
Dully Sykes ameuambia mtandao wa Times Fm moja kati ya sababu ambazo
zinambeba mwimbaji huyo na kumpeleka kwenye level ya juu ya mafanikio
kuwa ni kiu kubwa aliyonayo inayomfanya afanye kazi usiku na mchana huku
akiwasumbua maproducer bila kusubiri wamuite studio.
“Wasimuone Diamond anafanya vizuri, Diamond anafika mbali wakafikiria
Diamond anafanya kazi kwa kumsubiria hadi producer amuite studio, no
sio kweli. Diamond anashinda usiku kila siku studio.” Amesema Dully
Sykes.
Dully ameeleza kuwa hata yeye pia hukesha studio akifanya kazi na
ndio sababu inayomfanya aendelee kufanya vizuri tangu alipoanza muziki
bila kupotea na kwamba wasanii wengi wasiofanya hivyo huishia kuporomoka
na kudai kuwa walioko juu wanafanya uchawi.
Mwimbaji huyo ambaye ni mmiliki wa studio ya 4.12 ameongeza kuwa
akili ya kuwekeza kwenye vitega uchumi pindi uwapo juu ni moja kati ya
sababu zinazomsaidia msanii kuendelea kuwa juu kwa muda mrefu.
Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment