Breaking News
recent

Steve Nyerere afiwa na mwanae, ni mtoto wa pili kufariki

Mchekeshaji aliyejizolea umaarufu nchini kwa kumuigiza hayati baba wa taifa "Steve Nyerere Mangere" amefiwa na mtoto wake. Kwa mujibu wa majirani zake, mtoto huyo wa kiume ameishi siku mbili tangu azaliwe na kufariki. Huyo ni mtoto wa pili kufariki katika familia ya Steve na mkewe Zawadi.

"Sababu za kifo cha kwanza sijakijua, ila huyu wanasema atakuwa alivutwa wakati wa kuzaliwa, maana mtoto alikuwa mkubwa mno, sijajua alikua na kilo ngapi". kilisema chanzo hicho kilicho jirani na Steve. "Wa kwanza alifariki, wa pili yupo na huyu watatu amefariki", kwa mujibu wa chanzo hicho mazishi ya mtoto huyo yalifanyika jana.
Mohamed Jaku blog inampa pole Steve kwa msiba huo...
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.