Kwa longtime sasa hivi Tanzania
imeshuhudia magazeti mengi pamoja na stori za internet kwenye blogs, website na
facebook kuhusu Freemasons, kwa kiasi kikubwa baada ya hizo habari, picha
iliyojengeka kuhusu Freemasons ni kwamba ni dini ya kishetani.
Wametajwa
mastaa mbalimbali wa Tanzania pamoja na viongozi wa kisiasa kwamba nao
wamejiunga na dini hiyo akiwemo rais mstaafu wa Tanzania William Mkapa na Rais
Mwai Kibaki wa Kenya.
Exclusive
kwenye THE INTERVIEW ya CLOUDS TV Mtangazaji Gerald Hando amefanya interview na
Sir Andy Chande ambae alikua freemasons lakini kwa sasa amestaafu.
Moja kati ya mambo
aliyoyazungumzia ni pamoja na taarifa za Kibaki na Mkapa kuwemo kwenye hicho
chama, hapa namkariri akisema “Hakuna hata mmoja kati ya mkapa wala kibaki ambae
ni Freemason, nilipofika hapa mwaka 1950 katika biashara
zangu nilikutana na watu wengi
katika Nyanja mbalimbali ambao walikuwa wakiandaa chama cha freemasons ambao
walinialika kwenye vikao mbalimbali Uganda, Kenya, uingereza na kwingineko kama
Ghana na Khumasi ila nikastafu baada ya miaka 19 kufanya kazi na freemasons.
Sihusiki tena na freemasons
huku Tanzania, ila kama uingereza naenda mara kwa mara kwa sababu bado kuna
baadhi ya mashirika ninayofanyakazi nayo hadi sasa, Freemasons sio kama watu
wengi wanavyosikia au kuambiwa.. kuna tofauti”
Baadae hapahapa millardayo.com
nitakuletea interview kamili kuhusu mengine aliyosema kuhusu maana ya
Freemasons, kazi zao na mengine.

No comments:
Post a Comment