Kyle Glover ambae ni mtoto wa mke wa
zamani wa Mwimbaji Usher Raymond, amefariki dunia leo kutokana na kuumia kwenye
ajali ya pikipiki za kwenye maji maarufu kama
Jetski mwanzoni mwa mwezi huu huko Georgia Marekani.
Madaktari wametoa mashine zilizokua
zinasaidia kumuweka hai mtoto huyo aliekua na umri wa miaka 11 baada ya
kugundua kwamba majeraha aliyoyapata yasingeweza kutibika.
Kyle akiwa na rafiki yake wa kike
mwenye umri wa miaka 15
walipata ajali july 8 2012 huko Georgia
baada ya Inner tube waliyokuwemo iliyokua ikivutwa na boti kugongwa na Jetski
wakiwa kwenye maji na hivyo
kupata majeraha ya kichwa.
Hii ndio Jetski iliyowagonga hao watoto ambao walikua kwenye inner tube iliyokua ikivutwa na boti...!



No comments:
Post a Comment